Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka watumishi wa Idara ya Afya kuhakikisha wanazingatia matumizi sahihi ya mifumo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa wagonjwa
" daktari anapomwandikia dawa mgonjwa awe na uhakika kwamba hiyo dawa ipo na kama haipo amwambie mgonjwa hapohapo au amuandikie dawa nyingine inayoendana nahiyo siyo mgonjwa anafika dirisha la dawa anaambiwa hii dawa haipo" amesema Ludigija
Haya yamejiri leo Septemba 3,2024 wakati Kamati ya Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya walipokuwa wakikagua huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya.
Aidha Mkuu huyo amewataka kuboresha mifumo hiyo ili kuongeza mapato " huduma ikiwa nzuri wagonjwa wataongezeka mtapata mapato mengi kwahiyo imarisheni mifumo" amesema Ludugija
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Daktari Neema Gervas amesema Hospitali hiyo ilishaanza kutumia mifumo na wanaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mfumo.
Baada ya kukagua Hospitali kamati hiyo imekagua tenki la maji la Ngudu mjini ambapo wamewataka watumishi wa Idara ya maji kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.