Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amewataka viongozi wa dini kutoa elimu kwa waumini wao kuhusu ugonjwa wa kipindupindu Dalili zake na namna ya kujikinga
Ameyasema hayo leo Septemba 13,2024 kwenye kikao cha dharura kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri baada ya taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu Wilayani hapo
" hiki siyo kipindi cha kuwaonea watu aibu, tuambizane ukweli watu wajue kipindupindu ni hatari wajikinge, viongozi wa dini tumieni nafas zenu kufikisha ujumbe" amesema Ludigija
Katika kikao hicho wameshiriki Maafisa Afya kutoka Mkoani Mwanza ambao wameendelea kupita maeneo yenye mlipuko wa ugonjwa huo kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga.
Akiwasilisha taarifa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Zuber Mzige amesema vituo vya Afya sita vimeandaliwa kwaajili ya kupokea wagonjwa.
Wananchi wametakiwa kujikinga na gonjwa hilo kwa kuzingatia usafi wa vyoo, kunawa na maji tiririka mara kwa mara, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kwenda kituo cha Afya pindi wanapoona dalili za ugonjwa huo yaani kuharisha, kutapika na kuishiwa nguvu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.