Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wananchi wanaovamia eneo la kituo cha Afya Kikubiji kuacha mara moja tabia hiyo ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza
Ameyasema hayo Mei 13,2024 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho " niwatake wote wanaovamia eneo la kituo cha Afya na kufanya kazi zao za kilimo waache mara moja kwani eneo ni la Serikali kwa mujibu wa mahakama na kama Kuna mtu hakulidhika na uamuzi wa mahakama alipaswa kukata rufaa" amesema Ludigija
Aidha Mheshimiwa Ludigija amewataka wasimamizi wa ujenzi wa kituo hicho kuongeza kasi ya utekelezaji ili ifikapo mwezi Juni Kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi.
Pia amewaelekeza viongozi wa taasis za Tanesco na RUWASA kuhakikisha wanafikisha huduma za maji na umeme katika kituo hicho.
Naye meneja wa TARURA ameelelezwa kutengeneza Barabara inayoelelea kituoni hapo ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma pindi kituo kitakapoanza kutoa huduma.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.