Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija Leo Mei 8,2023 amezindua Zahanati ya Nyamatala iliyopo Kata ya Ngula.Akizindua Zahanati hiyo Mheshimiwa Ludigija amewataka Wananchi kuitumia Zahanati hiyo kupata huduma za Afya hasa wanawake wajawazito na watoto Ili kuepuka vifo vinavyoweza kuzuilika.
" wito wangu kwenu acheni tabia ya kupeleka wagonjwa kwa waganga wa jadi, yaani mtu akiugua kituo cha kwanza iwe kwenye Zahanati, tena waganga wa jadi muwe mabalozi akija kwenu mgojwa mshauri aende Hospitali kwanza, kwamfano wajawazito mnawapa dawa zinazosababisha madhara makubwa kwa watoto acheni hiyo tabia na atakayebainika anapokea wajawazito tutamchukulia hatua" Ludigija
Mkuu huyo ameitumia hadhara hiyo kuwaeleza Wananchi kupeleka watoto wao shuleni Ili kutokomeza ujinga na kuongeza wasomi
" hakikisheni mnasomesha watoto wenu, angalieni hawa vijana waliopangiwa kazi hapa Nyamatala wamesomeshwa na wazazi wao nanyie mtamani kuona watoto wenu wakiwa Madakitari,Walimu, wahandisi na wataalam wengine somesheni watoto" Ludigija
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo na amewashauri kulitumia ipasavyo kwa kuhakikisha wanapata huduma za Afya pia amewashauri kuitunza miundombinu ya Zahanati hiyo Ili idumu.
Wananchi wa Kijiji hicho wameishukuru Serikali kwa kuleta fedha millioni 50 kwaajili ya kukamilisha Zahanati hiyo "Kabla hatujapata hii Zahanati tulikuwa tunateseka kufuata huduma mbali na Kijiji na hiyo ilipelekea wanawake wengi kujifungulia nyumbani hivyo kusababisha wengine kufariki kwahiyo tunaishukuru Serikali kutukamilishia Zahanati hii" amesema Judith Elias
Zahanati ya Nyamatala ilianzishwa kwa nguvu za Wananchi na baadhi ya wafadhili wakiwemo kanisa la Baptist ambao walichangia zaidi ya millioni 50.
Aidha Mkuu wa Wilaya amefungua huduma za Afya katika Kituo cha Afya Isunga ambapo walipokea millioni 500 kwaajili ya ujenzi huo na jengo la wagonjwa wa nje,kichomea taka na Maabara vimekamilika na majengo ya wazazi na jengo la kufulia yamefikia hatua ya ukamilishaji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.