Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi S. Ngaga amesaini kitabu cha maombolezo ya Kitaifa ya Kifo cha Hayati Mhe. Dkt.JohnPombe Magufuli leo tarehe 19/03/2021 katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Aidha amewataka wanachi kuwa na moyo Mkuu,utulivu na mshikamano katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na kiongozi wetu mahili,shupavu Mcha Mungu,mtetezi wa wananchi wote.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndug.Nyakia Ally akisaini kitabu cha maombolezo
Viongozi mbalimbali na wananchi wamejitokeza kusaini kitabu cha maombolezo huku wakionyesha masikitiko na majonzi ya kuondokewa na kiongozi aliyependeka kutoka na uchapakazi wake,uhodari na ushujaa katika uongozi, "ni simanzi na majonzi makubwa kuondokewa na kiongozi aliyekuwa mtetezi wetu sisi wanyonge,ametusaidia vituvingi,watoto wetu wanasoma bure, huduma za Afya zilikuwa zimeimarishwa, bado tulikuwa tunatarajia maendeleo makubwa kutokana na ahadi zake sasa taa imezimika ni majonzi makubwa kwetu wananchi wa Kwimba" amesema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Peter Kabelelo
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mwalimu Emmanuel Katemi akisaini kitabu cha maombelezo.
Afisa Utumishi(W) Ndug.Joshua Mgoli akisaini kitabu cha Maombolezo.
Mananchi akisaini kitabu cha maombolezo,Ndug.Peter Kabelelo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.