“Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza waripoti shuleni wote asiwepo mtu wa kusingizia hana sare za shule au madaftari”
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi leo tarehe 27,Disemba 2022 kwenye ziara yake iliyolenga kukagua utekelezani wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari na ujenzi wa vituo vya Afya.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amewaelekeza wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni na atakayezembea kusimamia wanafunzi hao hatua za kisheria zitachuliwa dhidi yake.
Aidha Mheshimiwa Samizi ameshauri wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Maligisu wanaotokea samilunga na maeneo jirani wahamishiwe katika Shule mpya ya Sekondari Samilunga ili kuwapunguzia umbali wanaotembea kwenda Maligisu.
Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Sumve kinachojengwa kwa fedha za mapato ya ndani amepongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo. Vilevile Mkuu huyo amesisitiza huduma za Afya zianze kutolewa katika Kituo cha Afya Kadashi ili wananchi wa kata hiyo waepukane na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya akiwa ameambatana na kamati ya Usalama na Wataalam wa Halmashauri wamekagua Shule za sekondari Samilunga,Iseni,Tallo,Nyamigamba,kinoja,Sumve na Wala pamoja na Vituo vya Afya Kadashi, Isunga na Sumve.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.