Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Samizi amekemea tabia ya Wananchi kuvamia maeneo shule na kufanya shughuli za kilimo. Ameyàsema hayo leo tarehe 14, Novemba 2022 katika mkutano na Wananchi wa kijiji cha Ligembe.
"Mahakama ilishatoa maamuzi kuwa eneo ni mali ya Shule sasa wewe raia unayeona hukuridhika na maamuzi hayo rudi mahakamani lakini siyo kuwatisha walimu kwa mapanga, fimbo na siraha nyingine, nakemea tabia hiyo na atakayekamatwa anafanya vurugi kwenye eneo la shule hatua za kisheria zitachukuliwa" amesema Samizi
Mkuu huyo ameyasema hayo baada ya mgogoro wa ardhi kuibuka kati ya wanafamilia wa Busanda na Shule ya Ligembe, ambapo Mahakama ilishatoa hukumu iliyoelekeza kuwa eneo ni mali ya shule lakini familia hiyo inaonekana kutokubaliana na uamuzi wa mahakama.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi, na kufanya fujo na kuhatarisha usalama. Katika Mkutano huo wananchi wa kijiji cha Ligembe wameitaka familia ya Busanda kuacha kuvuruga amani katika kijiji hicho kwani wanaamini mgogoro uliisha baada ya mahakama kutoa hukumu
"mgogoro huu sisi tulishakaa tukaumaliza tumeshangaa kuona leo tunaitwa tena kuambiwa mgogoro ambao mahakama ilishaumaliza, sisi hatutaki kusikia, huu mgogoro haupo tunachotaka shule yetu isiingiliwe na mtu" amesema Isaya Yona mwananchi
Akitoa ufafanuzi juu ya hukumu iliyotolewa na mahakama Afisa Ardhi ( W) Ndugu Wicklif Benda amesema mahakama ilijiridhisha kuwa eneo ni mali ya shule baada ya kufatilia usajili wa shule ulioanza zaidi ya miaka 40 iliyopita na vigezo vingine vilivyobainisha kuwa eneo ni mali ya shule.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.