Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi akiwa ameambatana na kamati ya hamasa ya utoaji wa elimu ya Chanjo ya UVIKO-19 ya Mkoa na Wilaya wametoa elimu ya umuhimu wa chanjo hiyo kwa wananchi wa Kata ya Mantare kijiji cha Mwampulu na Mwanekeyi, Kata ya Bungulwa na Walla ambapo baada ya Wananchi kupata elimu hiyo watu 30 wamejitokeza kupata chanjo ya virusi vya corona.Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 05,Oktoba 2021.
Akiongea na Wananchi Mkuu wa Wilaya amesema chanjo ni salama hivyo wasiogope kuchanjwa kwani kila Mwananchi anapaswa kulinda Afya yake.
"kufa kupo ila hatupaswi kufa kizembe hivyo ni muhimu kuchanja ili kujihakikishia usalama wa Afya" amesema Samizi
Aidha akiongea na vijana waendesha Pikipiki amewashauri kutosikiliza maneno yasiyo sahihi yanayowafanya wahofie usalama wa Afya zao baada ya kuchanja.Amewahakikishia kuwa chanjo ni salama na amewashauri wachanje kwa kuwa kazi yao inawafanya kukutana na watu wengi wanaotoka maeneo tofauti hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi.
Baada ya kuchanja Wananchi hao wamepatiwa kadi zinazoonyesha kuwa wamejikinga na virusi vya corona.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.