Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameaswa kushiriki katika ujenzi wa madarasa, mradi unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO-19 ambapo madarasa 109 yanajengwa katika shule za Sekondari.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi leo tarehe 03/11/2021 katika baraza la Madiwani. Mheshimiwa Samizi amesisitiza kuwa Madiwani na viongozi wengine wote wanapaswa kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha nyingi ili kujenga madarasa ambayo yakikamilika yatapunguza au kuondoa kabisa changamoto ya upungufu wa madarasa katika baadhi ya Shule.
" tunachotakiwa kufanya ni kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za ujenzi wa madarasa kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa Serikali kupeleka fedha nyingi Nchi nzima kwa wakati mmoja lakini jambo hili limewezekana katika Awamu hii ya sita, hivyo niwaombe tushiriki kusimamia na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati". amesema Samizi
Katika Baraza hilo Waheshimiwa Madiwani wameweza kueleza jinsi tatizo la upungufu wa madarasa linavyoongezeka siku kwa siku baada ya mwitikio wa wanafunzi kujiunga na Elimu ya Sekondari kuwa mkubwa kutokana na Sera ya Elimu bila malipo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga amesema Serikali haijaishia kwenye ujenzi wa madarasa tu bali imelata milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya viwili yaani Kituo cha Afya Bungulwa ambacho ujenzi unaendelea na Kituo cha Afya Kikubiji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.