Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi amewashauri wakulima wote kuhakikisha wanalima Pamba kuanzia ekari tatu na kuendelea ili kuweza kutimiza lengo la kuzalisha tani elfu 30 kwa mwaka.Ameyasema hayo leo tarehe 07/11/2021 katika vijiji vya Ibindo, Kadashi,Nyashana, Bugandando,Mwabuchuma na Maligisu ambako Balozi wa Pamba Mhe.Aggrey Mwanri amepita kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba.
Akiongea na Wananchi baada ya kutoa elimu ya kilimo bora cha Pamba, Samizi amesema Kwimba iliwahi kuwa wazalishaji wakubwa wa Pamba na anataka kurudishe hiyo sifa, ili tuweze kukuza uchumi wetu.
" Nyie mnajua zamani Wilaya ya Kwimba ilikuwa mzarishaji mkubwa wa zao la Pamba mpaka ikaandikwa kwenye vitabu kama mzarishaji bora, hiyo sifa tunataka tiirudishe na hawatakuja watu wengine kuturudishia sifa yetu bali sisi wenyewe ndio tutairudisha, kwahiyo niwatake wakulima kwenda kulima Pamba kwa kufuata elimu hii na kila Mkulima aanze na hekari tatu ili tutimize malengo" amesema Samizi
Aidha Mhe.Mwanri amewashauri wakulima kubadirika na kulima kwa kufuata utaratibu wa kilimo cha kisasa cha kipimo cha 60 kwa 30 ambapo kutoka mstari mmoja hadi mwingine ni sentimita 60 na kutoka shimo moja la mbegu hadi jingine ni sentimita 30, Kupalilia kwa utaratibu unaotakiwa na kunyunyiza dawa kwa kuzingatia vipimo na matumizi bora ya mbolea hilo litairudisha Kwimba katika uzarishaji bora kama zamani.
Kilimo hiki cha kisasa ndicho kimewafanya Wakulima kutoka Nchi nyingi zinazolima Pamba kufanikiwa kwani kilimo kikizingatia vipimo Ekari moja inauwezo wa kutoa kilo 2500 za Pamba
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.