Ameyasema hayo leo tarehe 13,Novemba 2021 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu wakati akifunga kikao cha majumuisho ya zoezi la uhamasishaji wa kilimo bora cha pamba.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Johari Samizi amewasisitiza viongozi wote kwenda kufanya kazi ya kuhakikisha wakulima wote wanalima kama walivyofundishwa ili uzalishaji uwe wenye tija na ili lengo la kuzalisha tani elfu 30 liweze kufikiwa.
Amewataka watendaji kuhakikisha mbegu za pamba zinatolewa kwa wakulima na kuhakikisha zinaenda kupandwa kama lengo lilivyo, amewaonya wale wote watakaochukua mbegu za pamba na kwenda kuzifanyia kazi nyingine hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi yao.Mkuu huyo wa Wilaya amemuahidi Balozi kuwa elimu iliyotolewa itafanyiwa kazi na anatarajia mabadiriko makubwa katika kilimo cha zao la Pamba
" kutokana na elimu uliyoitoa Mheshimiwa Balozi nikuahidi tu kwamba tutaenda kuifanyia kazi na tunategemea kupitia elimu hii tuirudishe kwimba katika nafasi yake ya awali ya kuongoza zao la Pamba " amesema Samizi
Katika kikao hicho Balozi wa Pamba Tanzania Mhe. Aggrey Mwanri amewataka viongozi wote walioshiriki kikao hicho kwenda kusimamia maelekezo yaliyotolewa kwa wakulima ili wakulima hao waweze kulima kilimo chenye tija, pia amesisitiza kuwa wakulima wadogowadogo wanahitaji kushikwa mkono kwa kusimamiwa na kuelekezwa ili wafanye kilimo chenye manufaa.
" wakulima wadogowadogo ni kama mtoto mdogo ambaye anashikwa mkono ili kuvuka barabara kwaio tuwashike mkono wakulima wetu ili watoke kwenye kilimo kisicho na tija kilimo cha kushughulika waachane nacho ili walime kilimo cha mradi" amesema Mwanri
Naye Afisa kilimo wa Wilaya Magreth Kavalo amewapangia majukumu kwa kuwapanga katika vikosi kazi vitavyoweza kusimamia zoezi la kilimo bora cha Pamba, pia amewataka kwenda kuwahamasisha wakulima kulima mazao yote yakiwemo yale yanayostahimili mvua chache ili kuwe na uhakika wa kupata chakula kwa mwaka ujao, pia amesisitiza kuwa hali ya hewa inavyoonyesha mvua zitakuwa chache hivyo wananchi waambiwe umuhimu wa kupanda Pamba kwani zao hilo linastawi kwa mvua kidogo tu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.