Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari M. Samizi amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji na Wakuu wa Shule wanaoshiriki usimamizi wa utekelezaji wa miradi itokanayo na fedha za UVIKO-19 kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika tarehe 25 Oktoba,2021 kwenye Ukumbi wa Ngudu Sekondari ambapo amewaelekeza viongozi hao kuhakikisha madarasa yanayojengwa yanakamilika kwa fedha iliyoletwa na Serikali.Mkuu huyo amesisitiza kuwa hategemei kuona mradi wowote kuchelewa kukamilika kwa visingizio visivyo na tija,
" kila mradi utekelezwe kulingana na fedha iliyotengwa hakutakuwa na fedha za kuongezea rabda fedha zibaki ili zifanye kazi nyingine na mradi uwe umekamilika kwa viwango vinavyotakiwa" amesema Samizi
Aidha katika Kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Msanga amesisitiza uwajibikaji,uadilifu na uaminifu kwa watendaji na Walimu hao wanaoshiriki usimamizi wa miradi hiyo. Amewataka kutojishirikisha na vitendo vyovyote vitakavyopelekea miradi kukwama kwani hatua kali za kisheria zitachuliwa kwa yeyote atakayebainika.
Wilaya ya Kwimba imepokea kiasi cha shilingi Bilion 2.18 fedha za UVIKO-19 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 109 ya shule za Sekondari
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.