Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi awataka wazazi wote kuwanyonyesha watoto kwa miezi sita ya mwanzo bila kuwapatia chakula kingine.
Ameyasema hayo leo tarehe 02,Disemba 2021 kwenye hospitali ya Ngufu wakati akifanya uzinduzi wa mwezi wa Afya na lishe kwa Mtoto kwa kuwapatia watoto chanjo za matone ya viatamin A, Akiwahutubia wazazi waliofika kliniki kwaajili ya watoto wao amesema ili mtoto apate Afya na Lishe bora anatakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo bila kuchanganyiwa vyakula vingine, kufanya hivyo kunamfanya mtoto kuwa na Afya bora.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kufanya mambo yafuatayo:-
kunyonyesha watoto maziwa ya mama pee kwa miezi sita ya mwanzo, kuhamasisha ulaji na uzalishaji wa vyakula vyenye wingi wa vitamini na madini vinavyopatikana katika maeneo yetu, kuhamasisha ulaji wa vyakula vilivyoongezewa vitamin na madin, kuzingatia usafi wa mazingira na usalama wa chakula, na kuwapeleka watoto kwenye vituo vya Afya ili kufatilia ukuaji na maendeleo ya mtoto.
Aidha Mkuu huyo amesisitiza kuwa lengo la kuadhimisha mwezi wa lishe ni kuboresha Afya ya mtoto na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.
Maadhimisho ya mwezi wa Afya na lishe ya mtoto hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1, Disembà ambapo watoto wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano hupewa huduma mbalimbali za kiafya katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.