Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon Mkoga amewataka watumishi wa Halmashauri ya Kwimba kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma
"Watumishi wote fanyeni kazi, mimi nataka kuona kila mtu anawajibika katika eneo lake la kazi" amesema Mkoga
Haya yamejiri kwenye kikao cha Mkurugenzi na watumishi wa makao makuu ya Halmashauri kilichofanyika leo Septemba 4,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri kikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za watumishi.
Katika kikao hicho Mkoga amesisitiza uadilifu,nidhamu , utunzaji wa siri na kuwahi kazini " kuwahi kazini ni lazima" amesema
Aidha amewataka watumishi wote kushiriki katika ukusanyaji wa mapato, pia amewataka watumishi wote kujiandaa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Naye Afisa Utumishi (W) Bi. Jane Malongo ametumia wasaa huo kuwakumbusha watumishi majukumu yao huku akisisitiza matumizi ya mfumo wa upimaji PEPMIS.
Watumishi walioshiriki kikao hicho wameeleza changamoto na kero ambapo zimetolewa ufafauni huku nyingine zikielekezwa kwenye Idara husika kwaajili ya kutatuliwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.