Watendaji wa vijiji watakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma, haya yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon D. Mkoga kwenye kikao kilichofanyika leo Septemba 24,2024.
Mkurugenzi huyo amewataka watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badara yake wazingatie taratibu za utumishi " fanyeni kazì zenu kwa weledi, simamieni miradi na kazi zote mnazotakiwa kusimamia kila mtu ahakikishe anatimiza wajibu wake"
Watendaji hao wamesisitizwa kuweka fedha za makusanyo kwenye akaunti ya Halmashauri ili kuepuka vishawishi vya kutumia fedha ya serikali
" mkikusanya mapato hakikisheni hamkai na fedha nyumbani pelekeni Benki, sitarajii kuona mtumishi wa umma anasubiri kushurutishwa ndipo apeleke fedha benki"
Aidha Katibu Tawala Wilaya Ndugu Mohamed ametumia wasaa huo kuwataka watendaji kuendelea kuhamasisha wananchi kujenga vyoo ili kuepuka kipindupindu na magonjwa mengine ya mlipuko.
Naye Mganga Mkuu wa wilaya Dkt.Zuber amewataka watendaji hao kwenda kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa kuendelea kuchukua tahadhari.
Katika kikao hicho elim ya mpiga kura imetolewa huku watendaji wakihamasishwa kwenda kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Watendaji walioshiriki kikao hicho wamewasilisha kero zao huku wakuahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.