Idara ya Afya imetoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa makao makuu ya halmashauri ya Kwimba.Elimu hiyo imetolewa na Afisa Afya Silas Mboje katika ukumbi wa halmashauri, mtoa elimu ameelezea ugonjwa huo na dalili zake ambazo ni homa kali,kikohozi,kubanwa mbavu na kupumua kwa shida,kuumwa kichwa,mwili kuchoka pia ameeleza jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo nikwa kunawa mara kwa mara kwa maji yanayotirirka na sabuni au dawa ya kutakasia mikono, kuepuka mikusanyiko, kuepuka kusalimiana kwa kugusana mikono,kujikinga na kitambaa kizito au kiwiko wakati wa kukohoa na kupiga chafya,kuepuka kugusa macho, pua na mdomo, kukaa mbali angalau mita 1 au 2 na mtu mwenye homa au kikohozi mwenye historia ya kusafiri nje ya nchi.Aidha Mboje ameshauri watu kuzingatia kinga za ugonjwa huu ili kuepuka kuambukizwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.