Balozi wa Pamba Mheshimiwa Aggrey Mwanri akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Arch.Ngw'ilabuzu Ludigija Leo Februari 4,2023 wametembelea wananchi wa Kijiji cha Ilumba na Talaga ambapo wametoa elimu ya namna bora ya kumwagilia sumu ya kuuwa wadudu wanaoharibu Pamba.
Akiongea na wananchi hao Mwanri amewataka kufuata kanuni za upimaji wa dawa na kuzingatia hatua za kuchanganya dawa hizo na maji kulingana na ukubwa wa kifaa kinachotumika.
Aidha amewashauri wakulima kuacha kuchanganya Pamba na mazao mengine kwani kufanya hivyo nikukiuka kanuni za kilimo cha pamba pia kunapunguza kiwango cha pamba inayopatikana kwani wadudu wanaoshambulia mazao hayo yakishavunwa huhamia kwenye pamba na kuharibu kabisa zao hilo.
Naye Mkuu wa Wilaya ameitumia ziara hiyo kujitambulisha Kwa wananchi na kutoa rai yake Kwa wakulima wote kulima mazao ya chakula na mazao ya biashara Ili kukuza uchumi wa wananchi na Wilaya Kwa ujumla
" Pamoja na kulima mazao ya chakula, mwaka kesho Kila familia itatakiwa kuwa na shamba la Pamba lisilopungua heka moja, hiyo itatakiwa kulimwa bila kuchanganywa na mazao mengine" amesema Ludigija
Vilevile amewataka wananchi kuzingatia elimu inayotolewa na balozi wa Pamba pamoja na Maafisa ugani Ili iwasaidie kuokoa Pamba ambayo imeshaanza kushambuliwa na wadudu.
"Wakulima mmesikiliza maelekezo yanayotolewa hapa na Mwanri, wito wangu kwenu tumieni elimu hiyo kuokoa hii pamba ambayo inaonekana kuanza kushambuliwa, pia mkawe mabalozi Kwa wengine maana nyie mmeona hatua zote za kupulizia wafundisheni wengine Ili tuokoe pamba yetu"
Wakulima wameshauriwa kupulizia dawa muda ambao hakuna umande wala manyunyu au jua kali, bali muda mzuri ni kuanzia saa tatu hadi saa tano asubuhi na saa kumi na moja jion.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.