Katika kuadhimisha ya siku ya mtoto wa Afrika leo tarehe 16,Juni 2022 Elimu ya ukatili na unyanyasaji imetolewa kwa wanafunzi na wazazi katika Shule ya Msingi Mwañg'alanga.Mgeni rasmi Mwalumu Evarist Kawa amewataka wazazi na wanafunzi kuhakikisha wanapinga ukati kwa watoto na kutoa taarifa pindi waonapo dalili za ukatili kwa mtu yeyote.Mwalimu Kawa amesema tuupinge ukati kama kauli mbiu yetu inavyosema "Tuimarishe ulinzi wa mtoto,tokomeza ukatulia dhidi yake,jiandae kuhesabiwa"
Kawa amesisitiza swala la ukatili litokomezwe katika jamii " hii tabia ya kuwepo na matukio ya ukatili naomba ikome, watoto kutokupata haki zao za msingi ni moja ya ukatili,watoto hawapelekwi shule kupata Elimu na badala yake wanabaki majumbani kufanya kazi na wengine kwenda kuchunga mifugo, mzazi atakaye bainika kufanya vitendo vya ukatili kwa mtoto atachukuliwa sheria"
Aidha mgeni rasmi amewakumbusha wanafunzi pamoja na wazazi swala la utatuzi wa changamoto za miundombinu ya shule kuwa Serikali inatambua hivyo inaendelea kutekeleza ujenzi wa miyndombinu mbalimbali ili kuboresha idara ya Elimu. " ujenzi wa madarasa, miundombinu ya vyoo, ofisi za Walimu na miundombinu ya kunawia vinaendelea kutekelezwa kwahiyo watoto waende shule ili watumie miundombinu hiyo" amesema Kawa
Naye Mkuu wa dawati la jinsi Wilaya ya Kwimba Bi Nyasato Makongoro akatoa Elimu juu ya ukatili wa kijinsia" ukatili wa kijinsia ni hali ya kunyimwa haki yako ya msingi mfano kukatazwa kwenda shule,mtoto ukiona hupati haki yako ya msingi njoo utoe taarifa sisi Kama dawati la kijinsia tupo tutakusaidia usikubali kupoteza haki yako, na mtambue Sheria zipo zinazowalinda nyie kwahiyo na nyie mtoe taarifa muonapo hampati haki"
Sherehe hii imemalizika kwa kutoa zawadi kwa makundi matatu ambayo ni zawadi kwa mama mjamzito aliyehudhulia kilinki vizuri, zawadi kwa mtoto aliyehudhuria kilinki vizuri pamoja na kutoa msaada wa madaftari kwa wanafunzi wenye mazingira magumu na uhitaji maalumu,na ikumbukwe kuwa sherehe ya siku wa mtoto wa Afrika Tanzania huadhimishwa kitaifa kila baada ya miaka mitano.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.