Katika kuelekea kilele cha siku ya Mazingira ambayo Kidunia na Kitaifa inaadhimishwa tarehe 05 Juni,2021 Maafisa Mazingira wakishirikiana na wahandisi wa Wakala wa maji vijijini ( RUWASA) wametoa Elimu ya utunzaji wa Mazingira,matumizi ya nishati mbadala na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Maafisa hao wa Mazingira wamewaasa wanafunzi na Walimu wao kuwa mabalozi kwa wazazi wao na wananchi wote, wamewataka kwenda kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kutunza na kuhifadhi Mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Aidha Maafisa hao wamesisitiza upandaji wa Miti,kuacha Mita 60 kutoka vyanzo vya maji ( kutofanya shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji), kufanya usafi wa Mazingira na kutumia nishati ya gesi,umeme au mkaa unaotokana na takataka, wamewataka wanafunzi hao kuona uchungu wanapoona Miti ikikatwa kwaajili ya kuni na Mkaa.
Baadhi ya wanafunzi wameonekana kuwa mabalozi wa Mazingira kwani wamepanda Miti na wanaihudumia ili iweze kukua na kufanya Mazingira ya Shule kuwa na mandhari nzuri kwaajili ya kujisomea.
Siku ya Mazingira ina kaulimbiu isemayo " Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia" hivyo Wananchi wote mnashauriwa kutumia nishati mbadala kama gesi na umeme katika matumizi ya nyumbani ili kupunguza uharibifu wa Mazingira.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.