Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga ametoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
Elimu hiyo imetolewa leo kwenye kikao cha kamati ya maendeleo ya Kata ya Maligisu kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Maligisu
' Mwenyekiti wa kijiji na kitongoji hakikisheni mnatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha maana wasipojiandikisha hawataweza kupiga kura kwahiyo wahamasisheni wajiandikishe' Msanga
Bi. Msanga amewasisitiza viongozi wote walioshiriki kikao hicho kwenda kutoa elimu kwa wananchi ili muda utakapofika wa kuboresha taarifa kwenye daftari la mpiga kura wote waliofikia umri wa kupiga kura wajiandikishe
Katika kikao hicho Mkurugenzi amewataka viongozi wa vijiji na kata kutokuwa chanzo cha kukwamisha ukamilishaji wa miradi
" sitarajii kusikia kiongozi ndio chanzo cha mradi kutokamilika, mtu anayekwamisha ukamilishaji wa mradi huyo ni adui mkubwa"
Aidha amewataka watumishi wa umma kushiriki kwenye matukio ya kijamii " lazima tuishi kwa kutegemeana na kuhamasishana na sote tunaishi kwenye Jamii kwahiyo kama kuna michango ya maendeleo lazima tutoe maana maendeleo ya mahali popote yanaletwa na wanaoishi eneo hilo" amesema Msanga
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kadashi Mhe. Philimon Ndulu amemshukuru Mkurugenzi kwa maelekezo aliyotoa na ameahidi kwenda kuyatekeleza.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.