Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija. awaahidi ushirikiano wataalamu kutoka Amref wanaofanya kazi katika kitengo cha Fistula ya Uzazi ambao wamefika Wilayani Kwimba kutoa elimu kwa viongozi juu ya namna ya kuwasaidia wagonjwa wa fistula na jinsi ya kuwaibua.
Akiwasilisha taarifa Meneja wa mradi huo Ndugu Gaspery Misungwi amesema taasisi hiyo inaelekea kukamilisha mradi huo kwa awamu ya tatu ambao itakamilika mwezi oktoba 2025, ambapo mpaka sasa wametibu wagonjwa 12 kwa Wilaya ya Kwimba na 180 kati ya 284 wanaotarajiwa kutibiwa kwa mkoa wa Mwanza.
Wataalamu hao wameshauri wanawake wenye ugonjwa wa fistula kutojificha ndani au kukimbilia kwa waganga wa tiba asili wakizani wamelogwa badara yake waende hospitali ya Bugando ambapo watapata huduma ya upasuaji bure na baada ya kupata huduma watasaidiwa elimu ya ujasiriamali ili wakaweze kuendeleza maisha yao.
Fistula ya uzazi ni ugonjwa unaosababishwa na uzazi pingamizi anaoupata mama mjamzito wakati wa kujifungua pindi anapokosa huduma nzuri au usaidizi wa daktari wakati wa kujifungua, pia huwapata hasa wale wanaojifungulia nyumbani.
Wananchi wote wameshauriwa kutewatenga wagonjwa wa fistula wala kuwanyanyapa bali wasaidiwe kufika katika vituo vya afya ili wapate usaidizi wa kufika katika hospitali ya Bugando kwaajili ya upasuaji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.