Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameapishwa leo tarehe 02/12/2020, Hafla hii imefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.Katika Hafla hii Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga amewapongeza waheshimiwa Madiwani kwa nafasi waliyoipata ya kuteuliwa na kuchaguliwa pia Mkuu wa Wilaya amewashauri kufanya kazi ili kuchochea maendeleo ya Wilaya hii.
MKUU WA WILAYA YA KWIMBA MHE.SENYI S.NGAGA
Picha ya pamoja ya Madiwani na Viongozi wa Wilaya ya Kwimba
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bib. Pendo Malabeja.
Vilevile Ndug.Ally Nyakia Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba amewapongeza waheshimiwa Madiwani kwa kuchaguliwa pia akasisitiza uadilifu katika kazi,uwajibikaji na kusimamia upatikanaji wa mapato ya ndani na matumizi ya mapato.
Ndug.Ally Nyakia Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba.
Katika Hafla hiyo ya uapisho jumla ya Madiwani 40, (30 wakiwa wa kuchaguliwa na 10 wakuteuliwa) wameapishwa na wamefanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti ambapo Mhe.Thereza Jackson Lusangija Diwani wa kata ya Ngudu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri na Mhe.Lucy Cyprian Nchangwe Diwani vitimaalumu amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Thereza Jackson Lusangija( aliyesimama).
Mhe. Thereza Lusangija baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri amewashukuru Madiwani wote waliomchagua na ameomba ushirikiano na amesisitiza kila Mtu afanye kazi katika nafasi yake,aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ameahidi kufanya kazi zitakazochagiza maendeleo ili kuonekane tofauti na uongozi uliopita, pia amesema Halmashauri hii tangu ianzishwe haijawahi kuwa na Mwenyekiti Mwanamke hivyo nafasi aliyoipata ataitumia kufanya kazi za kimaendeleo kwa faida ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.