Katika harakati za kurahisisha uendeshaji wa vikao, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeamua kuachana na matumizi ya kablasha za karatasi kwenye vikao na kuhamia kwenye matumizi ya mfumo wa kidijital e - Board.
Mfumo huo umeanza kutumika tarehe 17 Aprili,2024 baada ya Halmashauri kununua vishikwambi vya Waheshimiwa Madiwani kwaajili ya matumizi ya mfumo huo, e- board ni mfumo unaofanya kazi kwa kutumia simu janja, kishikwambi au komputa.
Mfumo wa e - board unarahisisha na kuwezesha uandaaji na uratibu wa vikao ikiwa ni pamoja na kuandaa ajenda, kutuma mihutasari,na kuwezesha menejimenti kuandaa Taarifa za utendaji kazi kwa vipindi mbalimbali.
Akiongea na Waheshimiwa Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri Bi. Theleza Lusangija amesema " tulisubiri kwa muda mrefu na tulitamani sana kutumia mfumo ili tuepukane na matumizi ya karatasi pia mfumo huu unapunguza gharama za uendeshaji wa vikao kwahio tumefurahi kupata vishikwambi na tunaanza kutumia mfumo huu kwenye vikao vyote"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.