Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekabidhi pikipiki tatu kwa Watendaji wa Kata. Pikipiki hizo zimenunuliwa na Halmashauri kwa milioni 10,200,000 fedha za mapato ya ndani zikilenga kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuwarahisishia kazi Watendaji.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija ameipongeza Halmashauri kwa kuona umuhimu wa kuwanunulia usafiri Watendaji wa Kata , pia amewataka Watendaji waliokabidhiwa vyombo hivyo kwenda kuvitumia vizuri na vikawe Chachu katika kuongeza makusanyo
" Katumieni pikipiki hizi kwenda kufanya kazi zilizokusudiwa na tunatarajia mapato yataongeza katika Kata zenu maana mmerahisishiwa kazi, pia mzitunze vizuri siyo unampa mtu yeyote kuendesha hiyo ni mali ya Serikali lazima itunzwe vizuri" Ludigija
Akiwasilisha taarifa ya ununuzi wa vyombo hivyo Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amesema Halmashauri imenunua pikipiki hizo tatu kwa milioni 10,200,000 bajeti ya mwaka wa fedha uliopita na katika bajeti ijayo Halmashauri inatarajia kununua pikipiki tano lengo likiwa kurahisisha kazi za Watendaji na kuchagiza ukusanyaji wa mapato.
Makabidhiano hayo yamefanyika baada ya tathimini ya kikao cha lishe ambapo Mkuu wa Wilaya amewataka Watendaji wote kuhakikisha Kila Kijiji kinaadhimisha siku ya lishe ya Kijiji
" hatuwezi kuboresha lishe za watoto na wanawake wajawazito kama hatutazingatia haya maadhimisho ya siku ya lishe maana kupitia hiyo siku watu wanapata nafasi ya kujifunza namna ya kuandaa vyakula kwa kuzingatia mlo kamili na maelekezo ya lishe kwa watoto" Ludigija
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.