Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija ameipongeza Halmashauri kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi hali iliyopelekea Halmashauri kununua gari ( Lori) lililopokelewa leo, ameyasema hayo leo Mei 29,2024 kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya tatu 2023/24.
" niwapongeze kwa kazi kubwa mnayofanya hadi kufanikisha mapato ya ndani kutekeleza miradi mikubwa, haya mambo tulizoea kuyaona kwenye Halmashauri za manispaa na majiji lakini Kwimba mnayaweza hongereni sana" Ludigija
Nao Waheshimiwa Madiwani wameipongeza Halmashauri chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato hali iliyopelekea Halmashauri kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, ukmilishaji wa Maabara,bweni,ununuzi wa gari (lori), ujenzi wa jengo la kusubilia wagonjwa Hospitali ya Wilaya,ujenzi wa vibanda soko la Ngudu mjini na shughuli nyingine.
" niwapongeze wataalamu kwa kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato hili jambo liendelee maana Halmashauri yeti inategemea mapato ya ndani yanayotokana na ushuru wa mazao hivyo tuendelee kusimmia ili mapato yaongezeke lakini wanaokata ushuru wawazingatie wakulima wanaotoka kuvuna" amesema Mayala Sagini Diwani Mwandu
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka ya Halmashauri Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesema katika robo ya tatu Halmashauri imepokea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali pia imepokea magari ya wagonjwa ( ambulance) tatu, pia Halmashauri imenunua gari aina ya lori kwaajili ya kusaidia kazi mbalimbali za Halmashauri.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Ndugu Aziza Isimbula ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi " niwapongeze kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kutekeleza miradi mbalimbali inayoonyesha wazi kuwa mnatekeleza ilani ya CCM"
Katika Mkutano huo ameshiriki Mbunge wa Jimbo la Sumve Mheshimiwa Kasalali Mageni ambaye ameipongeza Halmashauri kwa kujenga kituo cha Afya Budushi Jimbo la Sumve kwa fedha za mapato ya ndani.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.