Halmashauri za Mkoa wa Mwanza zimeagizwa kusomesha walimu wa michezo wawili kwa kila Halmashauri kwa gharama ya Shilingi 1,040,000/= kwa kila mwalimu katika Chuo cha Michezo Malya kilichopo katika Mkoa wa Mwanza Wilayani Kwimba ili kukuza vipaji vya michezo kwa wanafunzi.
Maagizo hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Mwanza Mhe Elisha Hilary wakati wa kikao cha ALAT kilichofanyika Wilayani Kwimba tarehe 21 Disemba, 2017.
Akiongea chuoni hapo Mkuu wa chuo cha Michezo Malya Ndg Richard Timothy Maganga alisema nia na madhumuni ya chuo ni kutengeneza wataalamu wa michezo ili kutoa mafuzo na kuwa na usimamizi sahihi wa michezo katika maeneo yote nchini, ili kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo nchini.
Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Ndg Richard Timothy Maganga akitoa Taarifa ya Chuo kwa Wajumbe wa ALAT Tawi la Mkoa wa Mwanza.
Akiendelea kuchangia mada Mwenyekiti wa ALAT Mkoa Mhe. Hilary aliipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kulima zao la pamba kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kulima pamba kama zao kuu la biashara.
"Tunatarajia kupata kilo 40,800 kwa shamba lote la ekari 68 sawa na wastani wa kilo 600 kwa ekari ingawa tulikumbwa na changamoto kipindi cha upandaji baadhi ya eneo la shamba lilituwamisha maji na kusababisha mbegu kuoza.Pia katika kilimo hifadhi baadhi ya magugu sugu hayakudhibitiwa vizuri na hivyo kuongeza gharama za palizi".
Hayo yalisemwa na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kwimba Bi Magreth Kavalo wakati akisoma taarifa ya shamba la pamba la kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa wajumbe wa ALAT Mkoa wa Mwanza walipotembea shamba la mfano la watumishi Kilyaboya.
Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kwimba Bi Magreth Kavalo akisoma Taarifa ya Kilimo kwa Wajumbe wa ALAT Tawi la Mkoa wa Mwanza wakati wa Ziara ya kutembelea Shamba la Mfano la Watumishi Kilyaboya.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Wanga aliwaomba Wajumbe wa ALAT kuwa kikao kijacho kitakachofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kijadili mambo ya kubadilishana uzoefu katika ufanisi wa kazi mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri ikiwemo shughuli za miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Wanga akichangi Mada wakati wa Mkutano Mkuu wa ALAT.
Mkutano Mkuu wa ALAT Tawi la Mkoa wa Mwanza Ulifanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ukifuatiwa na Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.