Mkuu Wa Wilaya ya Kwimba Mhe Senyi S.Ngaga amewakabidhi wakulima wa pamba Wa chama cha msingi (AMCOS) shilembo kiasi cha milioni tano Fedha iliyookolewa na TAKUKURU kutoka Kwa Jamada A.Juma Afisa Masoko Wa kampuni ya AFRISIAN na Julius Masule karani wa AMCOS ya Shilembo,ambao kwa pamoja walikubaliana kuchepusha kiasi cha milioni tisa Fedha za wakulima wa pamba wa ushirika huo.
Akikabidhi Fedha hizo kwa wakulima Mkuu Wa Wilaya amesema Fedha hiyo itatolewa kwa awamu mbili kutokana na jinsi zinavyorudishwa hivyo zilizotolewa leo tarehe 19/08/2020 ni awamu ya kwanza,DC amesema Afisa huyo wa kampuni alifanya utapeli kwa kumsainisha karani wa AMCOS kupokea fedha kisha akaondoka na fedha hizo hivyo TAKUKURU wamefanya kazi kubwa ya kufanikisha urejeshwaji wa fedha hizo.Mkuu wa Wilaya amewaomba wakulima kuendelea na Kilimo na kuwa na imani kuwa fedha zote wanazodai zitalipwa hivyo wasikate tamaa ya kulima pamba.Aidha Mhe.Ngaga amewataka TAKUKURU kushugulikia AMCOS zote zinazodaiwa na wakulima ili zilipe madeni hayo kufikia tarehe 30/09/2020.
Pia DC ameshauri wataalamu wa ushirika kutoa elimu kwa viongozi wa AMCOS ili waweze kujisimamia na kusimamia fedha Kwa weledi unaotakiwa.
Akitoa taarifa fupi Ndugu Julian Augustine Kamanda Wa TAKUKURU (W) amesema hatua iliyochukuliwa ya kuokoa fedha hizo ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na serikali wa kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa makosa ya rushwa hawanufaiki na mazao ya rushwa na wanachukuliwa hatua za kisheria.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.