Sekta ya Afya Wilayani Kwimba katika kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa hasa huduma za mama na mtoto, mafunzo mbalimbali kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHW) yameendelea kutolewa yakiwemo mafunzo kwa mfumo wa LEAP.
LEAP ni mfumo unaomuwezesha muhudumu wa Afya ngazi ya jamii kujifunza na kufanya mitihani ya masomo mbalimbali yahusuyo Afya. Mfumo huu wa LEAP umeanzishwa na Shirika la Amref ili kurahisisha utoaji wa mafunzo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii.
“ mfumo huu unamuwezesha muhudumu wa Afya ngazi ya jamii kujifunza kwa kutumia simu yoyote kinachotakiwa tu eneo hilo liwe na mtandao wa kuwezesha kupiga simu na kutuma ujumbe, mfumo huu ni rahisi na umewetuwezesha kutoa mafunzo tukiwa mbali na wahudumu” alisema Gasper Gaitano Afisa TEHAMA kutoka Amref.
Aidha Afisa huyo anasema mfumo hauhitaji mtumiaji awe na elimu kubwa sana ndipo aweze kuutumia bali muhufumu anatakiwa ajue kusoma na kuandika tu.
Wakikagua matumizi ya mfumo huo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii maafisa TEHAMA kutoka TAMISEMI wameshauri pamoja na wahudumu kujifunza kupitia mfumo uwekwe mwongozo wa mafunzo hayo kwa wasimamizi wa vituo vya Afya utakaowawezesha kutatua changamoto pale zinapotokea kwa wahudumu wa Afya zinazohusiana na huduma wanazotoa kwa Wananchi.
Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wameendelea kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo yanayolenga Ustawi wa Mwanamke ikiwa nipamoja na kuboresha huduma za uzazi,elimu ya kupunguza au kuzuia vifo vya mama na mtoto,kutokomeza ukatili kwa watoto na huduma nyingine za kiafya.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.