Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga akipokea vifaa vya kuwashia umeme wa jua ( Sola) kutoka kwa wadau wa Afya Shirika la ICAP ambao wametoa Sola za kuwasha umeme kwenye vituo vya Afya na Zahanati 16.
Vifaa hivyo vimepokelewa leo tarehe 23, Septemba 2023 kwenye Hospitali ya Wilaya.Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi amelishukuru shirika la iCAP kwa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia vituo vya Afya kufanya kazi vizuri
" tunalishukuru sana shirika la iCAP kwa kutuletea vifaa hivi vitasaidia kupatikana kwa umeme ambao utarahisisha upatikanaji wa huduma maana sasa hivi vituo vya Afya vinatumia mifumo ambayo inahitaji umeme kwa hiyo vifaa hivi vitasaidia sana upatikanaji wa huduma kwa uhakika" Msanga
Akikabidhi vifaa hivyo Dr.Emmanuel Mkonye kutoka iCAP amesema Shirika linaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa hivyo wamekabidhi vifaa hivyo Ili visaidie kupatikana kwa umeme Ili mifumo ya kutunza takwimu za wagonjwa na kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana kwa uhakika.
Bi. Happiness amewataka Madakitari na wahudumu wa Afya watakao tumia vifaa hivyo kwenda kuvitumia vizuri na kuvitunza ili vilete tija iliyokusudiwa.
Vifaa vilivyokabidhiwa vinauwezo wa kuwasha umeme masaa 24 hivyo hakutakuwa na kipingamizi au kuzuizi cha wagonjwa kuhudumiwa kwa wakati kwenye vituo vya Afya.
Aidha Mkurugenzi ameliomba shirika hilo kutoishia hapo bali waone umuhimu wa kuleta Sola nyingine kwaajili ya Hospitali ya Wilaya ili kusaidia kupatikana kwa huduma kwa wakati pindi umeme unapokatika.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.