Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Mhandisi Msafiri Mtemi Simeoni amewahakikishia wahitimu wa Jeshi la Akiba (Mgambo) kupewa kipaumbele pindi nafasi za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zitakapotangazwa.
“Nafasi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zitakapotangazwa nitahakikisha wahitimu wote wa Jeshi la Akiba wenye sifa wanapewa kipaumbele kujiunga na Jeshi hilo”
Mhandisi Msafiri aliyasema hayo wakati wa ufungaji mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika tarehe 12/08/2017 katika kituo cha Ilula tarafa ya Nyamilama wilayani Kwimba
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Msafiri Simeoni akiongea na wahitimu wa Jeshi la Akiba (Mgambo) wakati wa ufungaji mafunzo ya awali
Muhitimu wa mafunzo hayo Bi Leah Benson alisema Katika mafunzo hayo wamejifunza masomo ya aina mbalimbali kama:-Uzalendo na utiifu, mbinu za kivita,utimamu wa mwili,ujanja wa porini,utambuzi, huduma ya kwanza na silaha ndogondogo.
Aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo yamewafanya wawe na utayari wakati wowote pindi wanapohitajika kutekeleza jukumu lolote la kitafa
Muhitimu wa mafunzo Bi Leah Benson akisoma risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Msafili Simeoni wakati wa ufungaji mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba (Mgambo)
Naye Diwani wa kata ya Ilula Mhe. Amosy Kyuga alimuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ambaye aliwakilishwa na Afisa Utumishi Mkuu Bibi Christina Bunini kuwasaidia wahitimu wa Jeshi hilo kupata vitambulisho vya Bima ya Afya ili viweze kuwasaidia kupata matibabu.
Aidha Bibi Christina Bunini kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba aliwaomba wahitimu hao kuwa na moyo wa uzalendo ili kuleta maendeleo katika wilaya ya Kwimba na Taifa kwa ujumla.
Kwa kuhitimisha sherehe hizo Afisa Tarafa ya Nyamilama Ndg.Joseph Mwikwabe aliwaambia wahitimu mafunzo kuwa mafunzo waliyoyapata wayatekeleze kwa vitendo ili wananchi wetu waishi salama na kulindwa salama.
Mafunzo ya Jeshi la Akiba yalianza rasmi tarehe 15/07/2016 yakiwa na idadi ya wanafunzi 115 wavulana 135 na wasichana 20. Mpaka tarehe 11/08/2017 jumla ya wahitimu waliofanikiwa kumaliza mafunzo hayo kwa hatua ya kwanza katika kituo cha Ilula ambapo 60 walikuwa wavulana 53 na wasichana 07.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.