Kamati ya fedha,uongozi na mipanga ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeipongeza TASAF kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kiwango kinachotakiwa. Wameyasema hayo kwenye ziara ya Kamati hiyo iliyokagua miradi mbalimbali ikiwemo miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF.
" niwapongeze wasimamizi wa miradi ya TASAF kwa usimamizi mzuri wa miradi, lakini tuendelee kuishikuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha za kutekeleza miradi hii, haya madarasa ya hii Shule shikizi yanaenda kuwa mkombozi kwani yatasaidia watoto kupata Elimu karibu na makazi yao" amesema Lameck Hole Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Katika ziara hiyo Kamati imekagua ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mwalulyeho ambao umefikia hatua za ukamilishaji, ujenzi umetekelezwa kwa milioni 250, ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo ya Shule shikizi ya Mwamaya ambayo yametekelezwa kwa milioni 80.5, ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri unaotekelezwa Kwa Bilioni 1.3 fedha za awamu ya kwanza, pia wamekagua uchakavu wa madarasa ya Shule ya msingi Mwang'hanga.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.