Kamati ya Afya,Elimu na Maji imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata mbalimbali.Katika kata ya Nyambiti kamati imetembelea shule ya sekondari Tallo na kuona ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa,ukamilishaji wa bwalo na jiko ,matundu 8 ya vyoo na mabweni mawili ambayo yamekamilika kwa ajili ya maandalizi ya kuanzisha kidato cha tano katika shule hiyo.Kamati imepongeza Halmashauri ya wilaya ya Kwimba kupitia idara ya Elimu,mipango na uongozi wa Kata na shule kwa kusimamia vizuri mradi huo na kuhimiza ari hii itumike kwa miradi mingine.
Aidha kamati hiyo imetembelea kata ya Ryoma kijiji cha Busule na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Busule ambapo jengo limepauliwa na ujenzi unaendelea,kamati imeshauri serikali ya kijiji hicho kuendeleza mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma za Afya.
Katika ziara hiyo kamati ilitembelea kata ya Mwabomba na kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ngogo,ujenzi umefikia hatua ya boma, uongozi wa kijiji umeshauriwa kukazana ili jengo hilo likamilike kwa wakati ili wananchi waepuke usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.