Kamati ya fedha, Uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba yafanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kujifunza namna shughuli mbalimba za ukusanyaji wa mapato katika migodi wa Wilaya hiyo inavyotekelezwà
Ziara hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 12-13 ,Aprili 2022 katika mgodi wa Nyandolwa ilikua na lengo la kujifunza mbinu mbalimbali ambazo wataalam wa Halmashauri hiyo wanazitumia ili kukusanya mapato katika migodi ya Wilaya hiyo.
Wajumbe wa kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Theleza Lusangija na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga, Waheshimiwa Madiwani na Wataalam walipata nafasi ya kujifunza utaratibu mzima wa shughuli zote zinazofanyika migodini ikiwemo uchimbaji wa madini,uchenjuaji na uuzaji wa dhàhabu na jinsi shughuli hizo zinavyosaidia katika kuinua uchumi wa Wilaya hiyo.
Katika Mgodi wa Nyandolwa Kamati iliweza kukutana na Mwenyekiti wa kamati ya ukusanyaji wa mapato katika mgodi huo Ndugu Ephafras Mazina ambaye aliweza kuelezea jinsi kazi za mgodi huo zinavyofanyika na jinsi wanavyoweza kudhibiti utoroshaji wa dhahabu na hivyo kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo
"Katika mgodi huu tunayo timu inayosimamia ukusanyaji wa mapato, tunahakikisha kila mfuko wa mawe unalipiwa ushuru, wanaojishughulisha na biashara zote wanalipa ushuru, wenye magari ya kubeba mizigo na vyombo vingine vya usafiri wanalipa ushuru kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na wanaokiuka utaratibu wanatozwa faini kwa mujibu wa sheria" alisema Mazina
Aidha kamati hiyo iliweza kutembelea maeneo mengine ikiwemo eneo inapojengwa hospitali ya Wilaya hiyo na kuona shughuli hiyo inavyotekelezwa, katika eneo hilo Mhandisi amabaye alielezea mbinu wanazotumia ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.
Wajumbe wa kamati hiyo waliweza kuzungumza na Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ndugu Stewart Makali ambaye aliwakaribisha katika Wilaya hiyo na akawaeleza kwa kifupi Shughuli za kibiashara zinazofanyika katika Wilaya hiyo, kisha wajumbe waliahidi kwenda kufanyia kazi yale mazuri yote waliyojifunza kutokana na ziara hiyo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.