Kamati ya Fedha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Theleza Lusangija imekagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, ziara hiyo imefanyika leo Mei 21,2024.
Kamati hiyo imekagua mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ambalo limefikia hatua ya kupaua na kujengwa Kuta, pia wamekagua ujenzi wa madarasa 10 namatundu 15 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Ngudu.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa madarasa manne katika Shule ya Sekondari Hungumalwa na ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Mwalujo.
Akiwasilisha taarifa za miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imeshapokea bilioni 1.7 ambapo bilioni 1.3 ilipokelewa Awamu ya Kwanza na milioni 400 imepokelewa awamu ya pili kwaajili ya ujenzi wa jengo la Utawala.
Baada ya ukaguzi wa miradi hiyo kamati imewapongeza wataalamu wa Halmashauri wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo ambapo wamepongeza kasi ya utekelezaji na ubora.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.