Katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufasaha, leo tarehe 29, Oktoba 2022 kamati ya fedha uongozi na mipango imefanya ziara katika maeneo mbalimbali kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo imekagua kikundi cha Wanawake Wakulima Isagala ambacho kikundi kilikopeshwa milioni 60 na Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba( mkopo usio na riba) ambapo kupitia fedha hiyo kikundi kimenunua trekta linalotumika kulima na kusafirisha mizigo, trekta hiyo imenunuliwa mwezi Septemba na kuanza kazi mwezi Oktoba. Tangu chombo hicho kianze kazi kimesaidia kuwaongezea kipato ambapo hadi kufikia leo kikundi kimekusanya milioni 4. Pia kikundi hicho kinajishughulisha na ufugaji wa ng'ombe ambapo kwa sasa wana ng'ombe 25.
" trekta hii inatumika kukodi kwa watu wanaohija kulima mashamba ambapo heka moja tunalima kwa shilingi 45,000 kwa hiyo inatusaidia maana ndani ya mwezi mmoja tumepata milioni nne japo mvua ingekuwa imeshaanza kunyesha tungepata fedha nyingi zaidi maana kazi zingekuwa nyingi" amesema Yasinta Heneriko katibu wa kikundi
Aidha kamati imekagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati Kilyaboya, mradi unaotekelezwa kwa milioni 152 fedha za mpango wa kunusuru kaya maskini. Hapo kamati imeshauri kasi ya utekelezaji wa mradi iongezwe ili mradi ukamilike kwa wakati.
Kamati haikuishia hapo imefika Shule ya Sekondari Nyamilama ambapo wamekagua ujenzi wa madarasa 12 kwa milioni 240 fedha kutoka Serikali kuu ambapo madarasa haya ni miongoni mwa madarasa 112 yanayotekelezwa kwa bilioni 2.4 fedha kutoka Serikali kuu. Katika mradi huu majengo yako hatua ya msingi na kamati imeshauri kasi ya utekelezaji wa miradi hii iongezwe ili miradi ikamilike kwa wakati.
Ikikamilisha ziara hiyo kamati imekagua ukamirishaji wa maabara katika Shule ya Sekondari igongwa ambapo milioni 30 ilipokelewa kwaajili ya kukamilisha maabara, maabara hiyo imekamilika na kuwekewa vifaa vyote vinavyotakiwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.