Kamati ya fedha,uongozi na mipango imefanya ziara katika mgodi wa madini Mhalo tarehe 21,May 2020 ili kuona jinsi mgodi huo unavyofanya kazi na jinsi wananchi wa eneo hilo wanavyoshiriki katika kazi hio.Kamati imetaka kujua kama mgodi huo unazingatia utunzaji wa mazingira na ulipaji wa kodi ya dhahabu hiyo.Mgodi una miaka 2 tangu uanzishwe na unamilikiwa na kikundi cha Mhalo mining group, Katibu wa mgodi ndugu. Sabana L.Salinja ameeleza jinsi mgodi unavyofanya kazi kuanzia uchimbaji hadi kupata madini. Mgodi umeweza kutoa huduma za kijamii katika kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kujenga ofisi ya kata,kuchangia saruji katika ujenzi wa madarasa ya shule,kuwalimia wazee hekari 12 za dengu na kwa sasa mgodi unajiandaa kujenga zahanati ya kijiji.Baada ya kupata maelezo hayo kamati imewataka viongozi wa kijiji na kata kusimamia kwa ufasaha mgodi huo ili kudhibiti utoroshwaji wa madini, ili kuongeza pato la Halmashauri.Aidha kamati imeshauri wawekezaji waongezeke katika mgodi huo ili kuongeza uzalishaji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.