Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kwimba Bibi Pendo A.Malabeja ameiomba kamati ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya Kwimba kuhamasisha masuala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.
Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Uhamasishaji kuhusu maswala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kwa kamati za lishe za Halmashauri tarehe 28 Agosti, 2017.
Aidha Bibi Pendo ameendelea kusema hatutegemei Kwimba kuzungumzia masuala ya utapiamlo
“Ni swala la aibu kuzungumzia maswala ya utapiamloa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ina vyakula vya aina mbalimbali na inaongoza kwa kuwa na ng’ombe wengi katika mkoa wa Mwanza”
Ni azma ya serikali kutokomeza utapiamlo ili kupata kizazi kitakachotupeleka kwenye Tanzania ya Viwanda. Hayo yamesemwa na DKT Laurent Mselle kutoka Taasisi ya Chakula Lishe Tanzania wakati akieleza malengo ya Mkutano wa Uhamasishaji kuhusu maswala ya Lishe kwa watoto,wasichana,wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.
Naye Bibi Abela Twin’omujuni kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania amesema tuwahimize wanawake wajawazito wajifungulie kwenye vituo vya afya ili waweze kupata elimu ya uzazi na kupunguza idadi ya akina mama wenye upungufu wa damu na uzito.
Bibi Abela Twin'omujuni kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akielezea umuhimu wa wanawake wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya Afya .
Akizungumza katika ufunguzi huo Bibi Mary Victor Kibona amehimiza masula ya lishe kwa watoto wachanga na wadogo
“Mtoto anyonye maziwa ya mama pekee na asipewe chakula chochote hata maji katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo kunyonyesha mtoto kunastawisha uhai, afya na maendeleo yake kiakili hivyo kumsaidia katika maisha ya baadaye,ikiemo elimu”
Hata hivyo aliendelea kuhimiza ulishaji wa vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miezi sita.
“Mtoto wenye umri zaidi ya miezi sita wapate chakula mchanganyiko na chenye madini ya chumvi kwa wingi na waasiishie kulishwa michuzi”
Bibi Mary Kibona kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe akihimiza masuala ya lishe kwa watoto wachanga na wadogo
Kwa kuhitimisha ufunguzi huo Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi Ngd.Jafari Magesa amesema ni lazima Halmashauri zielimishe jamii umuhimu wa matumizi ya vidonge vya kuongeza damu,kutoa na kusimamia dira ya serikali katika jamii na kuhahakikisha malengo ya huduma yanafikiwa kwa kushirikiana na wadau wengine kufikia nchi ya viwanda.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.