Katika kuadhimisha miaka 44 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kamati ya Siasa ya WIlaya ya Kwimba imefanya ziara ya siku mbili (3-4/02/2021) kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa,Katika ziara hiyo kamati imekagua na kupongeza juhudi zinazoonyeshwa na Halmashauri katika kuhakikisha miradi inakamilika na kamati imeshauri miradi isimamiwe kwa ufasaha na utekelezaji uzingatie muda uliokusudiwa na Wizara.Pongezi hizo zimetolewa na Ndug. Anatori Nshange Katibu wa Chama kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni miradi ya Elimu ikwemo ujenzi wa vyoo vya kisasa Shule ya msingi Kadashi,ujenzi wa Chuo cha VETA Ngudu na ujenzi wa bweni,vyoo na madarasa mawili shule ya sekondari Tallo, hapo kamati ilipongeza uongozi wa shule ya Tallo kwa usimamizi mzuri wa miradi iliyokamilika na inayoendelea kujengwa vilevile wajumbe wa kamati wameshauri kwa kuwa majengo yameboreshwa na taaluma iboreshwe kwa maana ya matokea kwa kidato ya pili,nne na sita.
Majengo ya chuo VETA
Vyoo vya Shule ya Msingi Kadashi
Bweni Tallo Sekondari
Kamati imetembelea miradi ya Afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo majengo manne yaani jengo la wagonjwa wa nje (OPD),Maabara,Utawa na jengo la mionzi vinaendelea kukamilishwa,pia wametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Kadashi ambapo mpaka sasa kuna majengo matatu jengo la wagonjwa wa nje,Maabara na jengo la Mama na Mtoto(jengo la wazazi), hapo kamati imeshauri kasi ya ujenzi wa kituo hicho iongezwe kwani wananchi wanahitaji kupata huduma kwenye Kituo hicho ili waepuke kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.
Jengo la OPD la Hospitali ya Wilaya
Jengo la wazazi Kituo cha Afya Kadashi
Vilevile kamati ilitembelea miradi ya maji ya Isunga-kadashi ambapo mradi ulishakamilika kwa zaidi ya asilimia 80 na wananchi wananufaika na mradi huo,pia mradi wa maji wa Shirima-Izizimba -Mhande hapo kamati iliwataka MWAUWASA kukamirisha mradi huo kwani wananchi wa maeneo hayo wanataabika kutafuta maji maeneo ya mbali vilevile walishauri ufumbuzi wa haraka ufanyike ili vifaa vilivyokosekana vya kumalizia mradi huo vipatikane na mradi ukamilike.
Tanki la maji Izizimba A
Tanki la maji Ngudu
Kliniki ya Mifugo
Kamati hiyo imekagua barabara za rami zenye urefu wa kilometa 1.2 na kushauri barabara hizo zitengenezwe baadhi ya maeneo yaliyobaki ili zikabidhiwe, na kamati imeshauri Kliniki ya Mifugo ianze kufanya kazi za kiushauri wakati vifaa vya kliniki vikisubiliwa.Wajumbe wakamati hiyo wamesisitiza kuwa Kantini ya Halmashauri ikamilike ili ianze kutumika na kuiongezea Halmashauri mapato.Aidha Katibu wa Chama amesisitiza kuwa kamati hiyo inachotaka kukiona ni utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo miradi yote inapaswa kukamilika ili malengo ya Chama yatimie.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.