KAMATI YA SIASA WILAYA YAMPONGEZA RAIS KWA KULETA FEDHA ZA MIRADI
Posted on: January 31st, 2025
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba Mhe. Sabana Salinje wamewapongeza wasimamizi wa miradi ya elimu, maji na Afya baada ya kufanya ziara leo Januari 31,2025 na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo
" nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi hii tumeona ujenzi wa Shule mpya mbili za sekondari ambazo zimekamilika kwa viwango vizuri, pia tumeona miradi mingine chuo cha michezo Malya shule ya msingi ya mchepuo wa kiingeleza, kisima cha maji na zahanati, niwapongeze sana wasimamizi wa miradi hii mmefanya kazi kubwa" Sabana
Katika ziara hiyo ameshiriki Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija ambaye ameihakikishia kamati hiyo kuendelea kusimamia na kufuatilua kwa karibu utekelezaji wa miradi yote na kuhakikisha kila mradi unakamilika kwa wakati.
Aidha Mheshimiwa Thereza Lusangija Mwenyekiti wa Halmashauri amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuleta fedha za miradi na amesisitiza kuwa miradi yote itakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi .
Naye Katibu wa chama cha Mapinduzi ndugu Aziza Isimbula ametumia wasaa huo kuwataka wananchi kufahamu kuwa katika awamu ya sita Serikali ya Rais Samia imefanya mambo makubwa hapa Wilayani Kwimba hivyo wananchi wanapaswa kumpongeza na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kuiletea Kwimba maendeleo
" kwanza Kwimba tunapendelewa sana miradi mingi na ya ghalama kubwa inatekelezwa Kwimba tunapaswa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali" Aziza