Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mheshimiwa Michael Masanja imefanya ziara Wilayani Kwimba leo Mei,24,2024.
Wakikagua miradi ya ujenzi wa Shule Mpya Bumyengeja,ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri, ujenzi wa kituo cha Afya Budushi na ujenzi wa Maabara na bweni Shule ya Sekondari Nyamilama wamepongeza wasimamizi wa miradi hiyo
" niwapongeze sana Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi mmefanya kazi kubwa sana miradi ni mizuri Inaubora pia thamani ya fedha inaonekana hongereni sana" amesema Masanja
Viongozi hao wa CCM wamewapongeza wananchi wa Budushi kwa kujitoa kununua kiwanja kilichotumika kujenga kituo cha Afya na kuchangia nguvu kazi wakati wa ujenzi wa kituo cha afya, pia amewashauri kuitunza miundombinu ya kituo hicho ili kidumu.
Akiwasilisha taarifa za miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kuleta fedha zinazotekeleza miradi hiyo.
Wananchi wa Sumve nao hawakubaki nyuma wameishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma za Afya pia wameipongeza Serikali kwa kujenga Shule Mpya Bumyengeja
" tunaishukuru sana Serikali kwa kujenga Shule imewasaidia watoto wetu hawatembei umbali mrefu kwenda Shule wanasoma hapa karibu" amesema Jesca Masanja
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amesema kuongezeka kwa miundombinu ya elimu kumehamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao pia utoro umepungua hivyo kupelekea Kwimba kupaa kwenye matokeo ya mitihani ya Kitaifa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.