"Hela za miradi tuziogope kama hela za sanda" haya yamesemwa na Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Mhe.Simon Mangelepa kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza ambapo alikuwa akimuwakirisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Akiongea katika ziara hiyo Mheshimiwa Mangelepa amewataka watu wote wanaosimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuogopa fedha hizo na wasimamie miradi kwa weredi ili malengo ya Mheshimiwa Rais yakamilike kama ilivyokusudiwa.
Aidha Mwenezi amempongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha za kuanzisha Shule mpya za Sekondari kitu kitakacho hamasisha watoto wengi kuendelea na masomo ya Sekondari kwani maeneo yanayojengwa Shule mpya yatawapunguzia umbali wa kutembea kwenda Shuleni,Mwenezi amewasisitiza Wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani miradi niyakwao
"simamieni, mshiriki ili kuhakikisha miradi inakamilika kama ilivyokusudiwa msiwaachie viongozi tu, hii miradi niyakwenu" amesema Mangelepa
Katika Ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni Ujenzi wa kituo cha Afya Isunga ambacho kilipokea milion 250 kwaajili ya kuanzisha majengo matatu ambapo limejengwa jengo la Wagonjwa wa nje(OPD), Maabara na kichomea taka. Mradi mwingine ni usambazaji wa umeme katika vijiji 55 vilivyokuwa bado havijapata huduma hiyo, ujenzi wa Daraja mradi uliotekelezwa chini ya TARURA, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Nkalalo ambapo miloni 470 zimeshapokelewa na ujenzi unaendelea, ujenzi wa Chuo cha VETA ambapo walipokea bilion 1.6 ya kuanzisha Chuo na sasa wamepokea milion 500 ya kukamilisha chuo hicho,na ukarabati wa Chuo cha Afya Ngudu ambapo walipokea milion 419.5 ili kufanya ukarabati ambapo tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwaka 1978 kilikuwa hakijawahi kufanyiwa ukarabati.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi Kwimba, pia ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kushiriki utekelezaji wa miradi kwa nguvu zao pale inapobidi na kwaulinzi amewataka Wananchi kutofumbia macho hali yoyote itakayoashiria kukwamisha miradi inayotekelezwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.