Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiongonzwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Mheshimiwa Sabana Salinja wamekagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Elimu,Afya, Utawala na kikundi cha walemavu.
Wakikagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mwalulyeho wameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha za kujenga Shule hiyo ambayo imeanza kutoa huduma tarehe 18 Septemba 2023, kukamilika kwa Shule hiyo kumewasaidia wanafunzi waliokuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya kilomita nane kitu kilichokuwa kinapelekea wanafunzi wengi hasa madarasa ya awali kushindwa kuhudhuria masomo yao.
Wajumbe hao wamekagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, hapo wamepongeza wataalamu na viongozi wote walioshiriki kusimamia utekelezaji wa mradi huo, pia wamesisitiza huduma za Afya ziboreshwe zaidi ili idadi ya Wananchi wanaopata huduma hapo iongezeke
" taarifa imeonyesha kuwa tangu muanze kutoa huduma katika Hospitali hii mapato yameongezeka sasa nishauri huduma ziboreshwe zaidi ili watu waje kupata huduma kwenye Hospitali hii na mapato yaongezeke zaidi" amesema Mwenyekiti wa CCM Mhe. Sabana
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija ameshiriki ziara hiyo naye amemtaka Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa jengo la utawala kuongeza kasi ya ujenzi huo ili jengo likamilike na kuanza kutumika.
Katika ziara hiyo miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini ( RUWASA) imekaguliwa, wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji ili miradi ya ujenzi wa tangi la maji Ligembe na Nkalalo yakamilike na yaanze kutoa huduma kwa wananchi.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa mabweni manne,madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mwamashimba, ujenzi wa kituo cha Afya Hungumalwa, kikundi cha walemavu Malemve, ujenzi wa daraja mto magogo, ujenzi wa kituo cha Afya Budushi, ujenzi wa mabweni mawili, madarasa manne na matundu ya vyoo sita Shule ya Sekondari Sumve na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Kadashi B mradi unaotekelezwa kwa milioni 540 fedha za mradi wa Boost.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.