Vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu wameshauriwa kuwa wabunifu zaidi katika shughuli zao za kiujasiliamari.Haya yamejitokeza wakati Kamati ya Uchumi ya Wilaya ya Kwimba ikifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo tarehe 19/04/2021.
Wakiongea na vikundi vya wajasiliamari vilivyopewa mikopo isiyo na riba na Halmashauri wamewapongeza kwa juhudi wanazozifanya za ujasiliamari na wamewashauri kuwa wabunifu zaidi kwa kuanzisha biashara zitakazowaongezea faida na kuwafanya wainuke zaidi kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ni miongoni mwa Wilaya zinazotekeleza agizo la Serikali la kutoa mikopo kwa vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu kutokana na agizo hilo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeshatoa mikopo zaidi ya Milioni 100 kwa mwaka huu wa fedha.
Vijana hao waliotembelewa na Kamati wameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mikopo isiyo na riba kwani kupitia fedha hizo wameweza kukuza miradi yao ikiwemo utengenezaji na uuzaji wa samani za ndani,kushona na kuuza Nguo, mikoba na vifaa vingine.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa choo cha Soko na kushauri kasi iongezwe ili mradi huo ukamilike kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma kama ilivyokusudiwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.