Kamati ya usalama ya Wilaya ya Kwimba ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu N. Ludigija wamepata mafunzo ya mfumo wa manunuzi ( Nest)
Akifungua mafunzo hayo Mhe. Ludigija amezitaka taasisi zote zilizopo Wilayani hapo kufanya taratibu za manunuzi kwa kutumia mfumo huo ili kuepuka changamoto na lawama kutoka kwa wafanya biashara
" mfumo huu ni mzuri kwa sababu haumkutanishi mfanya biashara na taasisi hii inaondoa lawama ya kusema kuna wazabuni wanapendelewa kwani wote wanaomba kwenye mfumo na mfumo ndio unachagua mzabuni"amesema Ludigija
Akitoa mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Kwimba ndiyo kinara wa matumizi ya mfumo wa Nest kwani inaongoza Nchi nzima, amesisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kutumia mfumo huo kwani tangu kuanzishwa kwa mfumo huo Halmashauri imepata faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupunguza ghalama za manunuzi ya vyakula vya wanafunzi shuleni
" kabla ya mfumo chakula cha wanafunzi shule ya Sekondari Mwamashimba kilikuwa kinanunuliwa kwa zaidi ya milioni 25 lakini baada ya mfumo chakula kinanunuliwa kwa milioni 16" amesema Msanga
Katika mafunzo hayo walikuwepo wawezeshaji wengine Deogratias Tulinawe Mkuu wa Kitengo cha manunuzi ambaye amewafundisha kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya umma inayozitaka taasisi zote kutumia mfumo huo na Esta Afisa Elimu Maalum Sekondari ambaye amefundisha namna mfumo unavyofanya kazi, kuandaa mpango wa manunuzi na kutangaza zabuni.
" haya mafunzo ni mazuri na yatatusaidia kusimamia taratibu za manunuzi kwa kuzingatia mfumo wa Nest" amesema Julian Augustin Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.