Kamati ya usalama ya Wilaya na wataalamu wa Halmashauri wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba wamefanya ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kwimba
Katika ziara hiyo miradi mbalimbali imetembelewa ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa na TASAF ambayo ni ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Kilyaboya ujenzi wa madarasa matatu na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Ng’uliku ambapo mradi utagharimu milioni 82 , ujenzi wa madarasa matatu na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Mwamitinjemradi unatekelezwa kwa milioni 81 na ujenzi wa madarasa matatu na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Kabale kwa milioni 80.6
Aidha kamati hiyo imekagua utekelezaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kikubiji mradi unatekelezwa kwa milion 500, ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita milion moja katika kijiji cha Hungumalwa mradi wenye gharama ya bilion 8.4 ambapo katika mradi huo tangi linajengwa, kusambaza maji kwa wakazi 5000 na kujenga ofisi na nyumba ya mlinzi. Vilevile wamekagua ujenzi wa barabara ya Mwamitinje.
Aidha vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vimetembelewa ambapo kikundi cha Mshikamano Ilula kilichokopeshwa milioni 15 na kikundi cha Tuinuane Sangu kilichokopeshwa milioni 7.6 wameelekezwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili waweze kukopeshwa kiasi kikubwa zaidi.
Mheshimiwa Samizi ameitumia ziara hiyo kuwaelekeza Wananchi kuendeleo kushiriki utekelezaji wa miradi, amekemea mauaji yanayoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali
“ sitaki kusikia mauaji yoyote yale niwaelekeze viongozi mauaji yakitokea tutakamata wananchi wote katika kitongoji kizima” amesema Samizi
Nao Wananchi wa vijiji vyote wakiwa ni pamoja na wananchi wa kijiji cha Kilyaboya wameishukuru Serikali kwa mradi wa zahanati na wameiomba Serikali kuendelea kupeleka miradi katika kijiji hicho kwani wananchi wote wako tayari kushiriki utekelezaji wa miradi katika kijiji chao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.