Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndg Andrea Ng’hwani kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kwimba ameahidi kabla ya Mwaka Fedha 2017/2018 kuisha ataakikisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ina miundombinu rafiki kwa watu wenye Ulemavu.
Ndg Andrea Ng’hwani aliyasema hayo wakati wa kikao cha kutoa mrejesho wa Mchakato wa Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Rasilimali na Matumizi ya Fedha za Umma kwa watu wenye Ulemavu kupitia Mradi wa “Zijue Haki zako Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017” kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama cha Walemavu tarehe 24 Octoba, 2017.
Akiwasilisha mada juu ya ufuatiliaj wa Mgawanyo na Matumizi ya Rasilimali za Umma katika sekta za Afya, Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali MNGON (Umoja wa NGO’S katika mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji aliishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji kwa ushirikiano waliouonyesha katika upatikanaji wa taarifa muhimu za Watu wenye Ulemavu.
Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali MNGON (Umoja wa NGO’S katika mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji akisoma Taarifa za Ufuatiliaji wa Mgawanyo na Matumizi ya Rasililmali za Umma katika Sekta ya Afya
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Ndg Vicent Bushaija kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji alikipongeza Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo Wilayani Kwimba kwa namna kinavyofanya kazi zake kwa bidii na kuishirikisha Serikali. Aliendelea kusema Halmashauri kwa upande wake itaendelea kutekeleza Sera ya Watu Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili kuhakikisha maslai ya Watu Wenye walemavu yanazingatiwa.
Aidha aliwataka watu wenye Ulemavu kutumia fursa mbalimbali zikiwemo za Mikopo inayotolewa na Halmashauri ili kuanzisha na kuendesha Miradi ya Kiuchumi ili kukuza kipato chao.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Ndg Vicent Bushaija akiongea na washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Matokeo ya Utekelezaji wa Shuguli za Mradi wa“Zijue Haki zako Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017”.
Katibu wa CHAWATA Wilayani Kwimba Ndg Andrew Sabuni alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kuwa Watu Wenye Ulemavu wa Viungo wawe wanahusishwa kwenye kamati mbalimbali za maamuzi kuanzia ngazi za vijiji hadi Halmashauri.
Mwenyekiti wa chama Chama cha Walemavu Wilayani Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa akichangia taarifa wakati wa kikao cha kutoa Mrejesho wa mchakato wa Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Matumizi ya Fedha za Umma kwa Watu Wenye Ulemavu (PETS).
Imam wa Msikiti wa Ngudu Ndg Nassor Husein Mokiwa alisema kwa kupitia Mradi wa Zijue Haki za Mtu Mwenye Ulemavu waumini wa dini ya kiislamu wamehamisika kutengeneza Miundombinu rafiki kwa Watu Wenye Ulemavu katika Msikiti wa Ngudu Mjini ili kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili Watu Wenye Ulemavu wakati wakuingia na kutoka Msikitini.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilayani Kwimba Ndg Nyerere Julias Musa aliiomba Serikali kupunguza Riba kwa mikopo inayotolewa kwa Watu Wenye Ulemavu ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mradi wa “Zijue Haki zako Mtu Mwenye Ulemavu kupitia Sera ya Afya ya 2017” Wilayani Kwimba Umetekelezwa katika kata ya Ngudu, Fukalo, Igongwa na Nkalalo ambapo wanufaika wa moja kwa moja ni walemavu 72 kati ya wanaume 32 wanawake 40 na wanufaika wasio wa moja kwa moja ni jamii wanaume wakiwa 370 na wanawake 227 jumla ni 597 waliofikiwa na elimu ya Ufuatiliaji wa Mgawanyo wa Rasilimali na Matumizi ya Fedha za Umma kwa watu wenye Ulemavu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.