Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri,Katibu Tawala wa Wilaya na Wakuu wa Idara na Vitengo wametoa kauli za pongezi na ahadi ya kufanyia kazi kile walichojifunza kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba. Haya yamejitokeza kwenya hafla fupi ya makabidhiano ya Mkurugenzi mstaafu Bib:Pendo Anangsye Malabeja na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Stamili A.Ndaro iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Kwimba.
Akiongea katika hafla hiyo Bib:Pendo Malabeja ametoa maneno ya nasaha kabla ya kukabidhi "fanyeni kazi kwa bidii,tekelezeni maelekezo ya Serikali,simamieni ukusanyaji wa mapato,pendaneni,endeleeni kushirikiano na fanyeni kazi kwa kufuata miongozo ya Serikali na wapendeni na kuwaelimisha wananchi kuhusu mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii" amesema Malabeja
Naye Katibu Tawala wa Wilaya Ndug.Nyakia Ally akawa na haya ya kusema"Mkurugenzi ulikuwa tunu kwetu, ulikuwa mlezi,Mzazi kuondoka kwako ni maumivu kwetu lakini ulichoweka kwetu ni tunu" Aidha Katibu Tawala amempongeza Mkurugenzi kwa kufikia hatua ya kustaafu na amewataka viongozi wanaoendelea na utumishi wa Umma kufanyia kazi yale yote waliyojifunza kutoka kwa Mkurugenzi huyo kwani yeye alikuwa Mwadilifu,mvumilivu,alifanya kazi kwa mujibu wa sheria,alidumisha mahusiano mazuri na watumishi na Wananchi wote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe.Theleza Lusangija amesema anamshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa malezii aliyowapatia na amewafundisha kazi Vilevile amewaomba Wakuu wa Idara na Vitengo kuendeleza ushirikiano aliokuwa akiuonyesha Mkurugenzi Mtendaji kwa Waheshimiwa Madiwani na Wananchi.
Aidha Afisa maendeleo ya jami kwa niaba ya wakuu wa Idara na Vitengo Bi.Rosalia Magoti amemshukuru Mkurugenzi kwa malezi na mafunzo waliyoyapata kutoka kwake na ameahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza kutokana na uongozi wake.
Mkurugenzi huyo amestaafu utumishi wa Umma baada ya kuwa ameitumikia Serikali katika maeneo mengi ikiwemo na Kwimba ambapo amefanyakazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kw miaka tisa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.