Wananchi wa Wilaya ya Kwimba wanaonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASSAF III) wameishukuru serikali kwa kuwapatia fedha za kujikimu kimaisha ,wananchi hao wamesema fedha walizopata zinawasaidia kuanzisha miradi midogomidogo kama ufugaji wa kuku,Mbuzi na kondoo vilevile fedha hizo zinawasaidia kujikimu katika swala la Afya na Elimu hasa kuwanunulia madaftari wanafunzi.
Mratibu wa TASSAF Ndug.Celestina Mushi amesema jumla ya shilingi 515,932,000 zimetolewa kwa kaya 6773 zilizopo kwenye mradi wa wanufaika wa TASSAF III,aidha Mratibu amewashauri wanufaika wa TASSAF kuzitumia fedha hizo kwa kufanya vitu vya kuwaongezea kipato.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.