Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ni miongoni mwa Wilaya ambazo zinapokea fedha kwaajili ya malipo ya Kaya maskini. Kwa mwezi Novemba hadi Februali Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepokea Milioni 901.6 kwaajili ya malipo ya awamu mbili.
Katika kutekeleza malipo hayo kaya zaidi ya elfu tisa zimepokea fedha hizo malipo hayo yalifanyika kuanzia tarehe 30 Machi 2022 hadi 05 April 2022.
Wakiongea kwa nyakati tofauti walengwa wa kaya maskini wamesema fedha hizo zinawasaidia kupata mahitani ya wanafunzi na kujikimu kimaisha, vilevile fedha hiyo zimewasaidia kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa Kuku, Mbuzi na kondoo.
Kupitia fedha hizo wapo walengwa ambao wameweza kubadilisha Nyumba zao za makazi kwa kujenga Nyumba za tofali na kuezeka kwa bati.
" Tasaf imenisaidia sana nilikua naishi kwenye nyumba ya nyasi sasa nimejenga nyumba ya tofali na nimeezeka kwa bati, naishukuru sana Serikali kwa kiendelea kutupatia fedha hizi" alisema Tabu Kwilabya
Naye Kaimu Mratibu wa Tasaf Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Kaali amesema Wilaya ilipokea milioni 901.6 kwaajili ya malipo kwa kaya 9831 lakini kaya zilizopokea fedha ni 9701 huku kaya 127 zikishindwa kupokea fedha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuhama, kusafiri na sababu nyingine.
Aidha walengwa wanaopokea fedha kwa njia ya mtandao wameonekana kufulahia huduma hiyo kwani wanapata fedha zao kwa wakati hivyo kusaidia kupata mahitaji yao kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.