Kaya 7836 zanufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF, ambapo jumla ya Shilingi 362,328,000 zimetolewa. Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekuwa ikiendelea kupokea Fedha kutoka Serikalini kwaajili ya kuzisaidia kaya maskini ili kujikimu kwa kupata mahitaji muhimu ya kiafya,Elimu na Chakula.Kupitia mpango huu watu wasiojiweza hasa wazee na watu wenye ulemavu wamekuwa wakinufaika sana.
Wakiongea kwa nyakati tofauti walengwa hao wa TASAF wamesema wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapatia fedha za kujikimu kwani kupitia fedha hizo wameweza kujenga nyumba na kuziezeka kwa mabati,wameweza kuanzisha ufugaji wa mbuzi,kuku,kondoo.Aidha Fedha hizo zinawasaidia kununua mahitaji ya wanafunzi kwa wale ambao wanawategemezi wanaosoma.
Walengwa hao wameshuhudia jinsi wanavyonufaika na mpango huo akiwemo Bi.Juliana Charles anasema "nimeweza kujikwamua kutoka kwenye nyumba ya nyasi sasa nimejenga nyumba ya tofali na bati pia nimeweka wapangaji vyumba viwili na fedha hizo zinaendelea kunisaidia kufanya maendeleo nawashauri walengwa wengine wakipata fedha hizi wafanye vitu vya maendeleo"
Walengwa hao wamesema fedha hizo zimewasaidia mambo mengi ikiwemo kupata huduma za matibabu kwani wengi wameweza kukata Bima ya Afya iCHF iliyoboreshwa hivyo wanapata huduma za Afya kwa urahisi.
Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya amesema jumla ya walengwa 74 hawakuweza kupokea Fedha zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo siku ya ugawaji wa fedha,kusafiri,na kuhama hivyo utaratibu wa kuwatafuta unaendelea kufanyika. Halmashauri ilipokea Shilingi 365,500,000 kwaajili ya malipo ya kaya 7910.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.